Viongozi wa CCM Kata ya Kindai Waendelea Kuzisaka Kura kwa Ari na Nguvu

                                      

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kindai wameendelea kuonesha mshikamano na ari ya hali ya juu katika kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi unaokuja. 

Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kata, Ndugu Omary Munda, wamekuwa mstari wa mbele kutafuta kura mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba kwa ajili ya wagombea wa CCM.

Katika mikutano hiyo ya mguu kwa mguu, Mwenyekiti Munda aliambatana na Kaimu Katibu wa Kata, Bi. Bernatta MartinMeneja wa Kampeni wa Kata, Ndugu Hamisi Kitila, pamoja na Mratibu kutoka CCM Wilaya, Ndugu Saidi Moshi. Pia walikuwepo Mjumbe wa Sekretarieti, Bi. Hawa WawaKatibu wa CCM Tawi la Kilambida, Ndugu Nakembetwa, pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Ndugu Hemedi Lisu.

Kwa umoja wao, viongozi hao walijitosa moja kwa moja kwa wananchi wa Kindai, wakieleza mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya serikali ya CCM na kuwaomba wananchi kuendelea kuiamini CCM kwa kuwapigia kura wagombea wake wote. Waliwahamasisha wananchi kuhakikisha kura za ushindi zinapatikana kwa:

  • Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
  • Mhe. Yagi Maulid Kiaratu kwa nafasi ya Ubunge, na
  • Mhe. Omary Salum Kinyeto kwa nafasi ya Udiwani wa Kata ya Kindai.

Viongozi hao walisema kuwa mshikamano huu wa viongozi wa CCM Kindai ni kielelezo cha umoja na mshikikano wa chama katika kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata maendeleo endelevu kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Wakaongeza kuwa, kila kura ya mwananchi wa Kindai ni kura ya maendeleo, amani na mshikamano wa kitaifa katika jamii yetu.

Na haya ni matukio kwa Picha Katika ziara hiyo.

Na Alifu Abdul Singida Kindai

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments