BERTHA NAKOMOLWA: NJOONI IKUNGI TUKAFUNGE KAMPENI KWA KISHINDO, TUKAIPIGIE CCM KURA YA USHINDI

                                   

Baada ya kufanya ziara za kusaka kura katika kata kwa kata, kijiji kwa kijiji na mtaa kwa mtaa mkoani Singida, Comrade Bertha Nakomolwa ameendelea kuwa sauti ya hamasa na mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akiwa ameonesha ari na uthubutu wa kipekee katika kampeni za chama, Nakomolwa amesema sasa ni wakati wa kukusanyika kwa pamoja wilayani Ikungi, ndani ya Jimbo la Ikungi Magharibi, kwa ajili ya kufunga kampeni kwa kishindo kikubwa kinachoashiria ushindi wa CCM katika uchaguzi unaotarajiwa.

“Tumezunguka kote Singida. Tumeona mapokezi makubwa, tumeshuhudia imani ya wananchi kwa CCM. Sasa ni wakati wa kuhitimisha safari yetu kwa kishindo. Njoo Ikungi tukafunge kampeni, kisha tarehe ya kupiga kura tukapige kwa nguvu zote. Tuitikie wito wa maendeleo kwa tiketi ya CCM,” alisema Nakomolwa kwa hamasa.

Wananchi wengi wameendelea kumpongeza kwa uongozi wake wa mfano na jitihada za kuunganisha makundi mbalimbali ya vijana, wanawake na wazee katika kuhamasisha amani na mshikamano wakati wa kipindi hiki cha kampeni.

Wito wa Bertha Nakomolwa unalenga kuhakikisha kuwa CCM inaendelea kuandika historia ya ushindi, huku wananchi wakiahidi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kuhakikisha “Kura zote ni za kijani”.

Kwa kauli mbiu yake isemayo “Kura ya CCM ni kura ya maendeleo, amani na umoja wa kitaifa,” Nakomolwa amekuwa chachu ya uamsho mpya wa kisiasa ndani ya Mkoa wa Singida

                                       



Na Abdul Bandola Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments