Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, ameonesha umahiri na uhodari mkubwa katika maandalizi ya uchaguzi kwa kuhakikisha kila kitu kiko sawa, mazingira ni salama na wananchi wako tayari kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Singida, Mhe. Dendego alisema maandalizi yote yamekamilika kwa ufanisi mkubwa, akisisitiza kuwa mkoa upo katika hali ya utulivu, na vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo tayari kulinda amani kabla, wakati, na baada ya uchaguzi.
Ameongeza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya mipango madhubuti na ushirikiano wa viongozi pamoja na wananchi, akiwataka wote kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na utulivu ili kuendeleza demokrasia na maendeleo ya Taifa.
![]() |
| “Tumejipanga kikamilifu, kila kitu kiko sawa. Wananchi wa Singida tungependa tuwe mfano wa uchaguzi wa amani na utulivu Tanzania,” alisema Mhe. Dendego. |
Kwa utendaji wake wenye maono, Halima Dendego ameendelea kujijengea heshima kama kiongozi mwenye misimamo thabiti, asiyeogopa majukumu, na mwenye dhamira ya dhati ya kulinda maslahi mapana ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Na Abdul Bandola Singida


0 Comments