Hapi na Nakomolwa Wazindua Hamasa, Mwigulu Atamba Iramba

                             

Katibu wa Wazazi Taifa Ally Hapi leo amehitimisha ziara yake mkoani Singida kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika kata ya Shelui, wilaya ya Iramba, akiwa sambamba na mgombea ubunge wa jimbo la Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba, na Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Singida, Bertha Nakomolwa.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, Hapi aliendelea kunadi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025 kushiriki uchaguzi kwa kuwachagua wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge hadi Udiwani.

Kwa upande wake, Mwigulu Nchemba aliahidi kuendeleza kasi ya maendeleo kwa kuwaletea wananchi miradi mikubwa ya barabara, elimu, afya na kilimo, akisisitiza kuwa “Iramba  ni ngome ya ushindi wa CCM, na maendeleo yataendelea kushamiri.

Nakomolwa, ambaye ni kiongozi wa wazazi mkoani Singida, alihimiza mshikamano wa wanachama na wapenzi wa CCM, akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha kura zote za “ndiyo” zinaelekezwa kwa wagombea wa chama hicho ili kulinda heshima ya ushindi wa kishindo mkoani Singida.

Baada ya mkutano huo, msafara wa Hapi uliendelea kuelekea mkoani Shinyanga kuendeleza hamasa na kampeni za chama.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments