Wimbi la kisiasa limeendelea kutikisa Wilaya ya Mkalama, huku wananchi wakitangaza wazi kuwa “Mkalama iko tayari... Mkalama imeamua kwenda na Jesca Kishoa.”
Kauli hiyo imeibuka kama sauti ya umoja wa wananchi wanaotambua kazi, uadilifu na ubunifu wa Jesca Kishoa, mwanasiasa kijana, jasiri na mwenye dira ya kuiletea Mkalama sura mpya ya maendeleo.
Wananchi wamemuelezea Jesca kama mwanasiasa mahili, anayejua kuwasiliana, kusikiliza na kusimamia hoja zenye tija kwa wananchi. Wameeleza kuwa kupitia kwake, Mkalama imepata kiongozi mwenye upeo mpana na dhamira ya kweli ya kutumikia watu wake bila ubaguzi.
“Jesca si mwanasiasa wa maneno, ni mwanamapinduzi wa vitendo. Anaona mbali, anaweka mikakati na anasimamia maendeleo kwa moyo wa kizalendo,” alisema mmoja wa wazee wa kijiji cha Mwanga wakati wa mkutano wa kampeni.
Katika mikutano yake, Jesca Kishoa ameendelea kusisitiza kuwa nguvu ya maendeleo ipo mikononi mwa wananchi, na ni kwa umoja na kura za kishindo ndipo Mkalama itazidi kung’ara katika dira ya maendeleo ya Taifa.
“Mkalama imeamua, safari hii ni ya kazi. Tunajenga upya kila sekta kwa kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Kishoa.
Wananchi wa Mkalama sasa wameweka wazi msimamo wao — wanakwenda na Jesca Kishoa kama ishara ya imani, matumaini na mabadiliko chanya yanayogusa maisha ya kila mwananchi.
Matukio kwa Picha
![]() |
Na Abdul Ramadhani Singida





0 Comments