Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Mkoa wa Singida, ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Itigi, amempongeza Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Singida, Bi. Bertha Nakomolwa, kwa uongozi wake madhubuti na jitihada za kuifanya Jumuiya ya Wazazi kuwa imara, hai na yenye ushawishi mkubwa katika mkoa wa Singida.
Akizungumza wakati wa tukio la kisiasa lililohusisha viongozi wa chama, wanachama na wananchi, MNEC huyo alisema kuwa mwenyekiti huyo amekuwa mfano wa kuigwa katika kuendeleza taswira chanya ya CCM kupitia matukio yenye kuhamasisha umoja, upendo na maendeleo.
Aidha, amesisitiza kuwa hatua zinazochukuliwa na Jumuiya ya Wazazi mkoani Singida katika kuinadi Ilani ya CCM na kuwaombea kura wagombea wote wa chama hicho ni ishara ya uzalendo na uelewa wa hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025.
![]() |
| “Tukiwa na viongozi makini kama hawa, ushindi wa CCM si hadithi bali ni hakika. Tunawaomba wananchi waendelee kuiamini CCM kwa kuwa ndiyo chama kinachotekeleza ahadi zake kwa vitendo,” aliongeza. |
Kwa upande wake, viongozi na wanachama waliohudhuria walipongeza ushirikiano wa viongozi hao wawili wakisema ni ishara ya umoja ndani ya chama na ni msingi wa ushindi mkubwa unaotarajiwa kwenye uchaguzi ujao.
Na Alifu Abdul Singida Itigi



0 Comments