Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida, Bertha Nakomolwa, ameendelea kuonyesha mfano wa uongozi imara na wa kizalendo kwa kuendelea kusaka kura za wagombea wa CCM katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Akiwa katika Jimbo la Ilongero, Nakomolwa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi na kuhakikisha wanawachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi, akisisitiza kuwa kupiga kura kwa CCM ni kupigia kura maendeleo, amani na ustawi wa jamii.
Amesema kuchagua CCM ni kuendeleza heshima ya taifa lenye utulivu, umoja na dira ya kweli ya maendeleo. Ameendelea kupita kijiji kwa kijiji, kata kwa kata na jimbo kwa jimbo, akinadi Ilani ya CCM na kuhamasisha wananchi kushiriki kwa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Bertha Nakomolwa ameendelea kuwahimiza viongozi wa ngazi zote za chama kuendelea kuwa karibu na wananchi na kuwasikiliza, akisema “CCM inasikiliza, inatekeleza na inaleta matokeo.”

0 Comments