WANANCHI TUTAOGA MVUA YA MAENDELEO, NIMEPANGA KUWATUMIKIA KWA DHATI” – MH. KINGU

Mgombea Ubunge la Ikungi Magharibi  Mheshimiwa Kingu, ameahidi kufanya kazi kwa bidii na moyo wa kujituma ili kuhakikisha wananchi wa Ikungi wanaona matokeo halisi ya maendeleo ndani ya miaka mitano ijayo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofurika wananchi wa kada zote, Mh. Kingu alisema dhamira yake ni kuibadilisha Ikungi kuwa kitovu cha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kijana.

“Wananchi wenzangu, ndani ya miaka hii mitano ijayo tutaoga mvua ya maendeleo. Nimepanga kuwahudumia kwa moyo wa dhati, kwa uaminifu na kwa vitendo. Tutaona barabara zetu zikiboreka, miradi ya maji ikiimarika, na vijana wakipata fursa za kiuchumi,” alisema kwa msisitizo.

Aliongeza kuwa, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imetoa dira na mwongozo wa maendeleo kwa kila kata, na jukumu lake ni kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo unafanyika kwa ufanisi mkubwa kwa manufaa ya wananchi wote bila ubaguzi.

“Sio ahadi za maneno, bali ni ahadi za matendo. Tutashirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuleta maendeleo ya kweli hapa Ikungi,” alisisitiza Mh. Kingu.

Wananchi waliohudhuria mkutano huo walionesha imani kubwa kwa Kingu, wakimpongeza kwa uadilifu, uaminifu na utendaji wake thabiti katika shughuli za kijamii.

“Tunaona ndani ya Kingu matumaini mapya ya maendeleo. Ni kijana mwenye maono, uchapakazi na moyo wa kujitolea kwa wananchi,” alisema Bi. Mwanaidi Mushi, mkazi wa Kijiji cha Ikungi.

Kampeni za Kingu zinaendelea kwa kasi, huku wakazi wa Ikungi wakiapa kumpa kura zote ili apeleke sauti yao na miradi yao mbele zaidi ya ilipo sasa.





Na Abdul Bandola Singida Ikungi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments