YAGI KIARATU AENDELEA KUISOGELEA JAMII — WAFANYABIASHARA WA SAMAKI WAMUOMBA AENDELEE KUWASOGELEA

Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Singida Mjini, Comrade Yagi Maulidi Kiaratu, akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Comrade Lucia Mwiru, leo wametembelea wavuvi na wauzaji wa samaki katika Mtaa wa Singida Munange.

Ziara hiyo imekuwa fursa muhimu ya kusikiliza changamoto za wananchi wanaojishughulisha na biashara hiyo, huku Yagi akipokea maoni yao kwa moyo wa uwazi na kuahidi kuyatolea majibu ya vitendo baada ya uchaguzi.

Katika mkutano huo wa kirafiki na kimaendeleo, Comrade Yagi Kiaratu aliwaomba wananchi kuendelea kuamini na kuiunga mkono CCM, akisisitiza umuhimu wa kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Urais, yeye Yagi Kiaratu kwa Ubunge, na Comrade Omary Salum Hamisi (Kinyeto) kwa nafasi ya Udiwani Kata ya Kindai.

“Changamoto zenu tutazitatua kwa pamoja. Serikali ya CCM imeonyesha nia, tumeona miradi, sasa tuendelee na kasi hii,” alisema Yagi.

Kadri siku za uchaguzi zikihesabika, ujumbe wa amani, umoja na maendeleo unaendelea kutamalaki Singida Mjini, huku wananchi wakionyesha imani kubwa kwa wagombea wa CCM.
Zimebaki siku tatu tu — CCM mbele kwa mbele




Na Abdul Bandola Singida Mjini

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments