Akiwa katika shina hilo lenye wanachama 150, Ndugu Kihongosi aliwashukuru wanachama na uongozi wa Shina Namba 7 kwa mshikamano, nidhamu na uongozi wao thabiti. Alisisitiza kuwa huo ndiyo utofauti wa CCM na vyama vingine, kwa kuzingatia muundo imara wa Chama, Katiba yake na uongozi madhubuti kuanzia ngazi ya taifa hadi mashinani.
Aidha, aliwasilisha salamu za Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kueleza kuwa hata yeye ameendelea kujifunza misingi ya uongozi bora kutoka kwa viongozi wa mashina, akitaja Shina Namba 7 kama mfano wa uongozi wa karibu na wananchi.
Amewahakikishia wananchi na wanachama wa shina hilo kuwa CCM itaendelea kuleta maendeleo.
Kazi na Utu tunasongambele.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)


0 Comments