Privacy Policy
About
Contact
HOME
AFYA
SIASA
HABARI
MICHEZO
MAKALA
BURUDANI
BIASHARA
TEKNOLOJIA
MAGAZETI LEO
Home
SIASA
Kihongosi Aendelea Kung’ara Singida, Apongeza Uongozi Madhubuti wa CCM Mkoa Chini ya Martha Mlata
Kihongosi Aendelea Kung’ara Singida, Apongeza Uongozi Madhubuti wa CCM Mkoa Chini ya Martha Mlata
Bandolamedia
January 21, 2026
Na Bandola Media – Singida
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Laban Kihongosi, ameendelea kuthibitisha dhamira ya chama ya kusimama karibu na wananchi, baada ya kupokelewa kwa shangwe wilayani Ilamba mkoani Singida (Misigili) katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi.
Akiwasili katika eneo hilo, Kihongosi alipokelewa na viongozi wa chama na serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, pamoja na makada, wanachama na wananchi waliojitokeza kwa wingi kuonesha mshikamano, imani na mapenzi yao kwa chama na uongozi wake.
Akizungumza na wananchi, Kihongosi aliusifu uongozi wa CCM Mkoa wa Singida kwa kufanya kazi kwa karibu na wananchi, kusimamia nidhamu ya chama na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa tija na uwazi.
CCM Singida imejipanga vizuri kuanzia ngazi ya mkoa hadi matawini. Huu ni ushahidi wa uongozi imara, unaojali wanachama na unaosimamia kwa vitendo ilani ya chama, alisema Kihongosi.
Katika nukuu nyingine, Kihongosi alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, kwa kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama, akieleza kuwa hatua hiyo imeendelea kukipa CCM nguvu na kukubalika kwa wananchi.
“Ndugu Martha Mlata ni kiongozi mwenye maono, msikivu na mchapa kazi. Amefanikiwa kujenga mshikamano mkubwa ndani ya chama, jambo linaloifanya CCM Singida iendelee kuwa imara na yenye mvuto kwa wananchi,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, alimpongeza Kihongosi kwa uongozi wake thabiti na ziara yenye tija, akieleza kuwa ujio wake umeongeza ari mpya kwa wanachama na viongozi wa chama mkoani humo.
Ujio wa Katibu wa NEC umetupa nguvu kubwa. Ametuonesha kwa vitendo kuwa uongozi wa juu wa chama upo karibu nasi na upo tayari kutatua changamoto zetu,” alisema Mlata.
Naye mmoja wa viongozi wa wilaya hiyo alisema ziara ya Kihongosi imekuwa chachu ya kuimarisha nidhamu, mshikamano na uwajibikaji miongoni mwa viongozi wa chama.
Ziara hii imetufungua macho na kutupa mwelekeo mpya wa namna ya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na kujali maslahi yao.
Ziara ya Kihongosi inalenga kukagua uhai wa chama katika ngazi za msingi, kuhimiza mshikamano, kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuimarisha utekelezaji wa Ilani ya CCM, sambamba na sera za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wa Ilamba Misigili wameeleza kuridhishwa na ziara hiyo, wakisema ni kielelezo cha uongozi unaosikiliza wananchi, unaochukua hatua na unaojenga matumaini mapya ya maendeleo.
Ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo inaendelea katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Singida, huku chama kikiendelea kujiimarisha na kujipanga kwa ushindi na maendeleo endelevu kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI
Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560
Post a Comment
0 Comments
TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2021, KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE
January 15, 2022
Shule na wanafunzi 10 bora Kitaifa Matokeo ya Upimaji Darasa la Nne,Twibhoki ya mkoani Mara yaziburuza shule zote 14,144
January 15, 2022
HAYA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA ( PSLE 2023 )
November 23, 2023
TANZIA: ALLY MTONI "SONSO" AMEPOTEZA MAISHA
February 11, 2022
UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDINZI (CCM) MKOA WA KIGOMA KUKAGUA MIRADI MBALI MBALI YA SERIKALI
January 15, 2022
MANYARA YAONGOZA TAKWIMU ZA UANDIKISHAJI WATOTO SHULE ZA AWALI, KATAVI YABURUZA MKIA
January 06, 2022
Bi Martha Mlata Amtembela Mwenyekiti Wa Kwanza Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Wa Singida.
February 23, 2023
HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 18,2021
November 17, 2021
RC. Singida aiomba Serikali kuweka kodi Mafuta ya kupikia kutoka nje ya...
March 02, 2023
WAZIRI MKUU AWASILI KATESH, ATOA POLE AENDA KUKAGUA ENEO LA TUKIO
December 04, 2023
Advertisement
BANDOLAMEDIA
Wasiliana Nasi
Name
Email
*
Message
*
TUFUATILIE MITANDAONI
2026
313
2025
1322
2024
1390
2023
1361
2022
1627
2021
946
Habari Zilizosomwa Zaidi
TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2021, KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE
January 15, 2022
Shule na wanafunzi 10 bora Kitaifa Matokeo ya Upimaji Darasa la Nne,Twibhoki ya mkoani Mara yaziburuza shule zote 14,144
January 15, 2022
HAYA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA ( PSLE 2023 )
November 23, 2023
TANZIA: ALLY MTONI "SONSO" AMEPOTEZA MAISHA
February 11, 2022
AFYA
3/AFYA/post-list
0 Comments