MSITA AINIKA MIRADI YA MAENDELEO ITIGI, AMPA HESHIMA KIHONGOSI KWA UONGOZI THABITI WA CCM

                                      

Mbunge wa Jimbo la Itigi na Mnec wa  CCM Mkoa wa Singida,  Yohana Msita, ameendelea kuonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu kwa kueleza kwa kina miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Jimbo la Itigi.

Akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika mjini Itigi, mbele ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndg. Kenan Laban Kihongosi, Msita alibainisha kuwa Jimbo la Itigi limepiga hatua kubwa kimaendeleo hususan katika sekta za elimu, afya, miundombinu ya barabara, maji safi na salama pamoja na huduma za kijamii.

Msita alieleza kuwa ujenzi na ukarabati wa shule, vituo vya afya na zahanati umeongeza upatikanaji wa huduma kwa wananchi, huku barabara zikiendelea kuboreshwa ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na kukuza uchumi wa wananchi wa Itigi.

Pamoja na mafanikio hayo, Mbunge huyo hakusita kueleza changamoto chache zinazoendelea kujitokeza ikiwemo kupanda na kushuka kwa bei za mazao hasa Dengu    pamoja na uboreshaji zaidi wa barabara za vijijini. Alisisitiza kuwa changamoto hizo zinaendelea kushughulikiwa kwa ushirikiano kati ya Serikali, Chama na wananchi.

Katika hotuba yake . Msita alimpongeza kwa dhati Katibu wa NEC Taifa, Ndg. Kenan Laban Kihongosi, kwa uongozi wake mahiri, maono makubwa na uwezo wake wa kukisemea Chama cha Mapinduzi kwa hoja, hekima na ujasiri. Alisema ziara ya Kihongosi imeleta hamasa mpya kwa wanachama wa CCM, kuimarisha mshikamano na kuendelea kukijenga chama kuwa imara na chenye kusikiliza wananchi.

Kwa upande wake, Kenan Laban Kihongosi aliwasisitiza wanachama wa CCM kuendelea kushikamana, kuilinda misingi ya chama na kusimamia utekelezaji wa Ilani kwa vitendo, akieleza kuwa CCM itaendelea kuwa chombo cha matumaini na maendeleo kwa Watanzania wote.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa chama na Serikali, makada wa CCM pamoja na mamia ya wananchi wa Itigi, ambapo ulihitimishwa kwa kauli mbiu na shangwe zilizoonesha imani kubwa kwa Chama cha Mapinduzi na uongozi wake.

Na Bandola Media – Itigi, Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments