YAGI KIARATU AIPONGEZA SERIKALI YA DKT. SAMIA KWA KUIMARISHA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI

                             

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Yagi Kiaratu, ameendelea kumshukuru Mungu kwa kuendelea kumpa afya njema, hekima na nguvu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kutokana na juhudi zake za kuwathamini wananchi pamoja na makundi mbalimbali nchini kupitia sera na mipango yenye tija kwa maendeleo ya jamii.

Mbunge huyo amesema Serikali chini ya uongozi wa Dkt. Samia imeendelea kuonesha dhamira ya kweli ya kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuboresha utaratibu wa mikopo ya asilimia kumi inayotolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika halmashauri mbalimbali nchini.

Ameeleza kuwa maboresho hayo yameongeza uwazi na urahisi wa upatikanaji wa mikopo, hatua inayowawezesha wananchi wengi zaidi kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza shughuli za uzalishaji mali pamoja na biashara ndogo na za kati.

Aidha, Yagi Kiaratu amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili iweze kuleta manufaa kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla. Amesisitiza umuhimu wa nidhamu ya matumizi ya fedha pamoja na kurejesha mikopo kwa wakati ili kuwapa nafasi wananchi wengine kunufaika na fursa hiyo muhimu.

Wananchi wa Jimbo la Singida Mjini wameendelea kumpongeza Mbunge huyo kwa namna anavyoendelea kuwa mstari wa mbele kuhamasisha maendeleo, kuwatetea wananchi na kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha fursa za kiuchumi zinawafikia makundi yote ya kijamii.

Kupitia kauli zake za busara na moyo wake wa kuwatumikia wananchi, Yagi Kiaratu ameendelea kuwa mfano wa uongozi unaojali maendeleo ya watu na ustawi wa jamii . 

Na hizi nipicha mbali mbali katika tukio hilo


































Na Abdul Ramadhani Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments