Katika kikao cha Bunge cha leo, Mbunge huyo alijikita zaidi kwenye sekta ya afya ambapo aliendelea kuuliza maswali yenye tija, yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, huku akisisitiza umuhimu wa Serikali kuendelea kuboresha huduma za afya katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Itigi.
Kupitia hoja zake makini na zenye maslahi mapana kwa wananchi, Msita ameendelea kuonekana kuwa sauti ya wananchi wa Itigi ambao wamekuwa wakihitaji maboresho zaidi katika huduma za hospitali, vituo vya afya, zahanati pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba na watumishi wa afya.
Wananchi wengi wa Jimbo la Itigi wameendelea kumpongeza Mbunge huyo kwa namna anavyoendelea kutumia nafasi yake ya uwakilishi kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi zinawasilishwa kwa nguvu na umakini mkubwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbali na kuzungumzia afya, Yohana Msita ameendelea kujijengea heshima kwa wananchi kutokana na msimamo wake wa kuwatanguliza wananchi mbele kwa kupaza sauti kuhusu maendeleo ya jimbo hilo katika sekta mbalimbali muhimu.
Wachambuzi wa masuala ya siasa na maendeleo wameeleza kuwa aina ya uwakilishi anaoufanya Mbunge Msita ni ishara ya kiongozi anayefahamu wajibu wake kwa wananchi, hasa pale anapoendelea kusimamia masuala nyeti yanayogusa ustawi wa jamii moja kwa moja.
Kwa hatua hiyo, Mbunge Yohana Msita anaendelea kuwa miongoni mwa viongozi wanaotajwa kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza changamoto zao na kuzipeleka kwenye vyombo vya maamuzi kwa lengo la kutafuta suluhisho la kudumu kwa maendeleo ya Itigi na Mkoa wa Singida kwa ujumla.

0 Comments