UONGOZI WA VITENDO: CHIEF THOMAS MGONTO AENDELEA KUANDIKA HISTORIA IKUNGI MASHARIKI KWA KUJALI WATU NA KUGUSA MAISHA YA WANANCHI

Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Chief Thomas Mgonto, ameendelea na ziara yake ya "Sikonga na Chief Thomas Mgonto", inayolenga kusikiliza wananchi, kutatua changamoto zao na kuimarisha maendeleo katika kata mbalimbali za jimbo hilo.

Akiwa katika Kata ya Lighwa, Mbunge Mgonto alitembelea Shule ya Sekondari Lighwa ambapo alipata fursa ya kuzungumza na walimu na wanafunzi. Katika mwendelezo wa ziara hiyo, aliingia darasani na kutoa somo pamoja na nasaha kwa wanafunzi, akiwahimiza kuweka elimu mbele, kuwa na nidhamu, kujituma katika masomo na kuamini kuwa wao ndiyo viongozi wa Tanzania ya kesho.

Baada ya shughuli hizo, Mbunge Mgonto alipokea taarifa za msiba wa mtoto wa Balozi aliyekuwa akisoma darasa la tano. Bila kusita, alielekea nyumbani kwa wafiwa ili kutoa pole na kushiriki kuwatia moyo familia pamoja na wananchi waliokusanyika kwenye msiba huo.

Akizungumza na waombolezaji, Chief Mgonto alitoa maneno ya faraja na kusisitiza umuhimu wa mshikamano katika nyakati za majonzi. Alieleza kuwa viongozi wanapaswa kuwa karibu na wananchi wao si tu wakati wa maendeleo na sherehe, bali pia wakati wa huzuni na majaribu.

Wananchi waliohudhuria walimpongeza Mbunge huyo kwa unyenyekevu wake na kwa kuonesha upendo wa kweli kwa wananchi bila kujali mazingira, wakisema uwepo wake umeleta faraja kubwa kwa familia iliyofiwa.

                                              

Katika kuendeleza dhamira yake ya kuinua vipaji vya vijana, Mbunge Mgonto pia alikabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa shule na makundi ya vijana katika Kata ya Lighwa. Hatua hiyo inalenga kuhamasisha ushiriki wa vijana katika michezo, kuimarisha afya zao na kuibua vipaji vitakavyoweza kulitangaza taifa.

Ziara ya "Sikonga na Chief Thomas Mgonto" imeendelea kuacha alama ya uongozi unaoweka mbele maslahi ya wananchi. Kupitia kusikiliza changamoto, kuhimiza elimu, kuendeleza michezo na kushiriki katika nyakati za furaha na huzuni za wananchi, Mbunge huyo ameendelea kujijengea heshima kama kiongozi anayegusa maisha ya watu moja kwa moja.

Kwa wengi katika Jimbo la Ikungi Mashariki, uongozi wa Chief Thomas Mgonto umeendelea kuwa mfano wa uongozi wa karibu na wananchi, unaotanguliza utu, mshikamano na maendeleo ya jamii.

Na Abdul Ramadhani Tanzania

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments