DR. DENIS NYIRAHA: LUCY SHEE NI HAZINA YA CHAMA NA SERIKALI

                                             

Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa, Dr. Denis Nyiraha, ameeleza namna Katibu Lucy Shee alivyokuwa na mchango mkubwa katika safari yake ya kisiasa, akimtaja kuwa zaidi ya kiongozi, bali pia mama mlezi na mwalimu aliyemjenga katika masuala ya siasa na uongozi.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Bandola Media, Dr. Nyiraha amesema katika kipindi chote walichofanya kazi pamoja, amejifunza mambo mengi kutoka kwa Lucy Shee, huku akisisitiza kuwa mchango wake umeendelea kuwa sehemu muhimu ya safari yake ya kisiasa hadi kufikia hatua aliyonayo sasa.

Katibu wetu na mama yangu Lucy Shee, katika muda wote tuliofanya kazi pamoja tumefanya kazi vyema. Kwangu amekuwa kama mama mlezi na mwalimu wangu wa kisiasa. Hata hapa nilipo, mchango wake kwangu ni mkubwa sana,” amesema Dr. Nyiraha.

Dr. Nyiraha ameongeza kuwa mabadiliko ya majukumu au hatua mpya katika maisha ya uongozi hayapaswi kutafsiriwa kama mwisho wa safari, bali yanaweza kuwa daraja kuelekea fursa na majukumu makubwa zaidi.

Binafsi naamini hili ni daraja la kufika sehemu kubwa zaidi. Naendelea kuamini wewe ni hazina kwa Chama na Serikali yetu. Huko mbeleni kuna heri na mema zaidi kuliko sasa,” amesema.

Aidha, Dr. Nyiraha ametoa shukrani zake kwa Lucy Shee kwa mchango wake katika safari yake ya kisiasa, akimtakia baraka na mafanikio katika hatua zinazofuata.

“Nakushukuru sana na ubarikiwe sana,” amesema Dr. Nyiraha.

Kauli hiyo inaakisi umuhimu wa malezi ya kisiasa, uzoefu, mshikamano na uendelezaji wa viongozi ndani ya taasisi, ambapo viongozi wenye uzoefu hutoa nafasi kwa wengine kujifunza, kukua na kuendeleza misingi ya uongozi kwa manufaa ya chama na jamii.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments