KLABU ya Barcelona ipo katika mazungumzo na Inter Miami ya Marekani kuhusu Lionel Messi kurejea klabu hiyo kucheza mechi moja ya mwisho kwenye wanja wa Camp Nou.
Rais wa Barca Joan Laporta anataka fowadi huyo gwiji kucheza klabu itakaporejea kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wao mpya. (El Nacional – Spain)
Messi alijiunga na Inter Miami ya Marekani Julai 2023 akitokea Barcelona ambapo tayari ameshinda Kombe la Ligi Agosti, 2023.
Kwa sasa Barcelona ipo Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.
Ukarabati wa uwanja huo utakaokuwa na na paa kubwa zaidi barani ulaya ulianza mwisho wa simu wa 2022-2023.
Mwisho wa ukarabati umepangwa kuwa Juni 2026, ingawa Barcelona huenda ikarejea kabla ya tarehe hiyo.
SOMA: Barcelona yagoma kuuza 7 majira ya joto
Wakati ukarabati ukiendelea uwanja wa Manispaa ya Barcelona wa Olímpic Lluís Companys wenye uwezo wa mashabiki 54,000 ndio unaotumiwa na klabu hiyo kama uwanja wa nyumbani.
Utakapokamlika Camp Nou utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 105,000 huku ukiwa na muonekano wa kisasa zaidi.

Uwanja huo unakadiriwa kugharimu pauni milioni 1.5 utakapokamilika.
Kwingineko katika tetesi za usajili Liverpool inasita kufikia bei ya pauni milioni 50.5 ya Juventus ‘Bianconeri’ kwa ajili ya kumsajili beki Gleison Bremer na hivyo ipo tayari kutoa ofa kwa Bianconeri ya kubadilishana na mchezaji ambaye hajatajwa kama sehemu ya mpango wa uhamisho. (Todo Fichajes – Spain)
Manchester United ni miongoni mwa vilabu vilivyotuma maombi mwishoni kwa ajili ya Xavi Simons wa PSG , ambaye badala atajiunga tena na RB Leipzig kwa mkopo msimu wa 2024/25. (TBR Football)
Atletico Madrid inakaribia kufikia makubaliano kumsajili Conor Gallagher kutoka Chelsea, huku vipengele vichache vikibaki kukamilisha uhamisho. (Fabrizio Romano)
0 Comments