Na Jackline Kuwanda,Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samiah Suluh Hasan atongoza waombolezaji kuuga na kutoa heshima za mwisho kwa mwilii wa hayati Dkt John Pombe Magufuli Rais wa awamu ya tano katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amesema Mkoa umepewa heshima na dhamana ya kuandaa shughuli ya maombolezo na mazishi kitaifa machi 22 mwaka huu.
‘’heshima hii tuliyopewa imezingatia nafasi aliyoipa mkoa wa Dodoma wakati wa uhai wake hasa kwa kubeba jukumu la kutekeleza azimio la siku nyingi la kuifanya Dodoma kuwa makao ya nchi na serikali’’Dkt Mahenge
Aidha amewahimiza wakazi Mkoani hapa kushiriki wingi katika shughuli ya maombolezo .
‘’Shughuli za kusaini kitabu cha maombolezo limeanza leo ,serikali imeandaa utaratibu mzuri wa viongozi ,wananchi na makundi mbalimali kushiriki kusaini kitabu hiki na itakuwa ni uwanja wa Nyerere Square’’Dkt Mahenge
Dkt Mahenge amesema, viongozi watakao shiriki ni pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ally Husein Mwinyi ,viongozi wa kitaifa ,viongozi wa Jumuiya,Taasisi za kimataifa ,Mabalozi na Viongozi kutoka nchi mbalimali.
Hatahivyo Dkt Mahenge amesema ulinzi na usalama umeimarishwa katika maeneo yote Mkoani hapa.
0 Comments