NAMUNGO FC KAMILI KUIVAA RAJA CLUB KOMBE LA SHIRIKISHO

 Hemed Morroco, Kocha Mkuu wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Raja Club Athletics.

Mchezo wa leo Machi 10 ni hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Huu ni msimu wa kwanza kwa Namungo kushiriki mashindano ya kimataifa na kutinga hatua hii kubwa ambayo ni rekodi ya kujivunia kwa Namungo ambayo inapeperusha bendera ya Tanzania. 

Morocco amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu ila watapambana kupata matokeo chanya.

Tupo kwa ajili ya Tanzania hivyo kazi yetu itakuwa ni kusaka ushindi licha ya ushindani ambao upo na hilo lipo wazi.

Kikubwa mashabiki watuombee dua ili tuanze vizuri na wachezaji pia wapo na morali kubwa katika kusaka matokeo," .

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments