Recent-Post

Madiwani wamsimamisha kazi mtumishi Bukombe, mwingine aonywa


 Watumishi wawili wa idara ya afya halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita wamekutwa na makosa baada ya mashauri yao ya nidhamu kutolewa uamuzi na baraza la madiwani ambapo mmoja amesimamishwa  kazi na mwingine kupewa onyo kali.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Bukombe,  Yusuph Mohamed amewataja watumishi hao kuwa ni Paschal Nungula wa hospitali ya Wilaya ya Bukombe aliyesimamishwa kazi kwa utoro kazini na ofisa muuguzi msaidizi wa hospitali hiyo,  Yusita Madaha ambaye ameonywa na kurejeshwa kazini.

Mohamed amesema uamuzi huo umefikiwa na madiwani baada ya kupitia mashauri  ya nidhamu  ya watumishi hao na kubaini mmoja anastahili kusimamishwa kazi na mwingine kuonywa.

Awali baraza la madiwani walikubaliana huduma ya kliniki na uzazi zianze katika  zahanati ya kijiji cha Ng'anzo ili kuwapunguzia adha wananchi kutembea umbari mrefu kwenda Ushirombo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,  Said Nkumba alimuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Lutengano Mwalwiba  aliwataka watumishi wa umma  kuhudumia wananchi kwa kufuata maadili, kanuni, sheria na taratibu za utumishi wa umma.

Post a Comment

0 Comments