Recent-Post

Mbeya City yaanza na Gym kwa mzuka mwingi

 

Mbeya.Kikosi cha Mbeya City kimeanza mazoezi ya viungo (Gym) tayari kwa maandalizi rasmi ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

Timu hiyo ambayo ilinusurika kushuka daraja msimu uliopita dakika za mwisho, tayari imeanza kujifua ili kujiweka sawa na mikikimikiki ya msimu ujao.

Mwanaspoti imefika mazoezini kwa vijana hao wa Jijini hapa na kushuhudia kikosi cha nyota 22 wakiongozwa na Kocha Mkuu wao, Mathias Lule wakijifua zaidi, huku wakionekana kuwa na morari zaidi.

Pia mbali na Kocha huyo, gazeti hili lilimuona baunsa mmoja ambaye jina lake halikupatikana haraka akiwa siliasi kutoa maelekezo kwa wachezaji wakati matizi yakiendelea na muda mwingine akiongoza jalamba hiyo.

Hata hivyo Meneja wa timu hiyo, Mwagane Yeya hakutaka kuchukuliwa chochote akidai kuwa bado hawajawa tayari kuruhusu habari za timu hiyo kutangazwa hadi kesho Jumanne.

"Umefikaje huku? Ok Ila tunaomba usichukue  chochote hadi kesho kwa sasa bado hatujaruhusu japokuwa tayari tuko mwishoni  kukamilisha mambo ya usajili tukimaliza hata leo tutaruhusu," amesema Yeya.


Post a Comment

0 Comments