Recent-Post

TAIFA STARS KAZI INAENDELEA

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia ambapo ina mechi mbili za kucheza ndani ya mwezi Septemba.

Michezo hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ni dhidi ya DR Congo na Madagascar itakayochezwa Septemba 2 na Septemba 7, 2021.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen ilikuwa ikifanya mazoezi hayo katika Viwanja vya JK Park ambapo kulikuwa na program kadhaa zilizoandaliwa na benchi la ufundi.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwepo mazoezini ni pamoja na Simon Msuva, Erasto Nyoni, Feisal Salum, Metacha Mnata,Mzamiru Yassin, Idd Seleman, Mudhathir Yahaya pamoja na Ramadhan Kabwili.

Post a Comment

0 Comments