
Ni Simba ambao walitwaa Ngao ya Jamii msimu ulioyeyuka wa 2020/12 kwa ushindi mbele ya Namungo wameweka wazi kuwa wanahitaji kutetea taji hilo kama ilivyo kawaida jambo ambalo limejibiwa na mabosi wa Yanga.
Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba aliliambia Championi Jumatatu kuwa mpango mkubwa ni katika kutwaa mataji yote ambayo waliyatwaa msimu uliopita ikiwa ni pamoja na Ngao ya Jamii.
"Tunahitaji kuonyesha kwamba tunauwezo na nguvu ipo katika kutimiza yale tuliyopanga kwa vitendo, tunahitaji kutwaa Ngao ya Jamii, taji la ligi na mengine yote ambayo tutashiriki kikubwa ni kufanya vizuri na tupo tayari, " alisema Mangungu.
Kwa upande wa Yanga kupitia kwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara alisema kuwa kwa namna ambavyo wamesajili wanahitaji kuchukua kila kikombe ikiwa ni pamoja na taji la Ngao ya Jamii.
0 Comments