Recent-Post

YANGA YAPANIA KUPINDUA MEZA KIBABE NIGERIA


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuelekea katika mchezo wao wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United watakwenda Nigeria kupindua meza.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ngoma ilisoma Yanga 0-1 Yanga na kufanya wawakilishi hao wa Tanzania kuanza kwa kucechemea mchezo wa kwanza.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa wanamatumaini makubwa ya kupata matokeo katika mchezo wa marudio utakaochezwa Nigeria.

Uwezo tunao na nia tunayo, jambo moja tu ambalo tunakwenda kulifanya ni kumpiga mpinzani wetu na tutafanya jambo ambalo litaisimamisha Afrika na dunia ya michezo,".

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Septemba 19 na ikipoteza Yanga mchezo huo safari yake katika Ligi ya Mabingwa itakuwa imeishia hapo na ikishinda mabao zaidi ya mawili bila kuruhusu kufungwa watapenya hatua inayofuata.

Post a Comment

0 Comments