Madiwani Tandahimba wahimizwa kuhamasisha chanjo ya Uvico-19

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitama Baisa Abdallah Baisa amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kuhamasisha wananchi kuchanja chanjo ya Uvico-19.

Akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani amesema  pamoja na mwitikio mkubwa wa wananchi kupata chanjo lakini madiwani wanapaswa kuwa chachu ya kuendelea kuhamasisha wananchi.

Halmashauari hiyo imeelezwa kufajnya vizuri kwenye suala la uhamasishaji wa chanjo ya Uvico-19 na kuhamasisha katika maeneo ya mikusanyiko.

Nae Diwani wa kata ya Luaga, Rehema Liute  amesema wananchi wamekuwa wakipewa elimu ya umuhimu wa chanjo.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments