Wananchi wachangishana kujenga nyumba ya daktari


Mkuu wa wilaya ya Mlele,Filberto Sanga akisukuma baiskeli iliyobeba matofali kupeleka kwenye ujenzi wa nyumba ya Mganga Mfawidhi zahanati ya Masigo mradi ulioibuliwa na wananchi,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mlele, Teresia Irafay. Picha na Mary Clemence

Wananchi wa kijiji cha Masigo  wilayani  Mlele wamechanga fedha na vifaa vya ujenzi  kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya daktari  ili kunusuru maisha ya wagonjwa nyakati za usiku  kutokana na daktari huyo  kuishi mbali na eneo la kazi.

Wakizungumza na Mwananchi baadhi ya wananchi hao wameeleza adha wanayoipata kutokana na ukosefu wa nyumba ya mganga mfawidhi kuwa  wagonjwa na wajawazito wanapohitaji huduma usiku inawalazimu kutembea umbali wa kilometa tisa kwenda kituo cha afya Inyonga.

Ester Deus mkazi wa kijiji hicho amesema katika zahanati hiyo huduma zinatolewa mchana pekee hali ambayo inawaathiri wagonjwa hususani akimama wajawazito wanaohitaji huduma za kujifungua usiku.

“Mganga anaishi Inyonga anafanya kazi mchana tu anaondoka, usiku tunapata shida sana kuwasafirisha wajawazito kwenda Inyonga wakati mwingine wanajifungulia njiani lolote linatokea."

“Tukakubaliana  kuchangia na  fedha  zingine zilitokana na ushuru wa mavuno ya msitu wa kijijini  kwasasa  tumeanza ujenzi wa msingi ili ikikamilika aishi hapa," amesema.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Teresia Irafay  amewapongeza wananchi wa kijiji hicho kujitolea kuanzisha ujenzi huo na kushiriki kikamilifu akidai kuwa vijiji vingine viige mfano huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments