Watanzania 725 wapoteza maisha kwa Uviko-19

Watanzania 725 wamefariki duniani Kutokana na ugonjwa wa Uviko-19 tangu ulipoingia nchini mapema mwaka jana.

Idadi hiyo ni kati ya watu 26,164 waliothibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo kati ya hao 25, 330 walipona

Takwimu hizo zimetolewa leo Jumatano Novemba 10, 2021 bungeni na Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel wakati anajibu swali la mbunge wa viti Maalum Halima Mdee.

Katika swali la msingi Mdee ameuliza ni Watanzania wangapi wameugua Uviko-19 tangu ulipoingia nchini na akahoji Fedha kiasi gani zimetumika.

“Sh158 bilioni zimetumika kununua vifaa mbalimbali ikiwepo mitambo 19 ya kuzalisha hewa ya oksijeni yenye uwezo wa kuzalisha mitungi 20 hadi 300 ambapo mitambo saba ishasimikwa na mitambo 12 ipo katika hatua ya usimikaji” amesema Naibu Waziri Mollel

Akizungumzia gharama za upimaji amesema kipimo kwa mtu mmoja ni dola 135 ambapo Serikali inatoza dola 50  huku ikichangia dola 85 kwa kila anayepima.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments