WAZIRI MCHENGERWA AJIRA ZOTE ZINAZOOMBWA ZIFANYIWE KAZI NA SEKRETARIETI YA AJIRA NA SI KWINGINEKO

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakati akizindua bodi hiyo jijini Dodoma. 


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akielezea majukumu ya ofisi yake wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma. 


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma. 


Mwenyekiti wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bibi Sophia Kaduma akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa mara baada ya kuzindua bodi hiyo jijini Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuizindua bodi hiyo jijini Dodoma. 

.................................................................... 

Na.Alex Sonna,Dodoma 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohamed Mchengerwa,ameagiza mchakato wa ajira katika taasisi zote za umma nchini uratibiwe na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kama chombo huru ili kuleta uwazi na kuwezesha haki kutendeka. 

Waziri Mchengerwa ametoa agizo hilo wakati akizundua Bodi ya nne ya wajumbe wa sekretarieti ya ajira, jijini Dodoma. 

Mchengerwa amesema kuwa hivi sasa ajira zote zitapitia katika sekretarieti hiyo ili kupunguza,Rushwa,ukabila,udini na undugu ambao ulikithiri katika baadhi ya taasisi na idara mbalimbali za serikali. 

Aidha ametaka Sekretariati ya Ajira kupitia Katibu Mkuu na Naibu wake kwenda kuliondoa hilo ili kuweka uwazi wakati wa kutoa ajira. 

“Kuna baadhi ya taasisi zilianza kuajiri wenyewe naomba hili jukumu lichukuliwe na wizara na lifanyiwe kazi kwa uwazi na usawa,”amesema Mchengerwa 

Mhe. Mchengerwa amesema kuwa baada ya maelekezo aliyoyatoa, hategemei kusikia taasisi yoyote ya umma inafanya mchakato wa ajira bila kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 

Waziri Mchengerwa amewataka Wajumbe wa Bodi aliyoizindua, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi kwani wameaminiwa na Serikali na ndio maana wakapewa nafasi hizo ili kuisaidia Serikali kupata watumishi wenye uwezo ambao watatoa mchango kwa maendeleo ya taifa. 

Hata hivyo Mchengerwa ,amewataka viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa pia na wasio wa kuteuliwa kuacha kukaa ofisini bali wanatakiwa kuwajibika na kuwa wabunifu. 

Pia ametoa rai kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kuangalia namna ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wanajiunga na vyuo vya Veta na vile vya maendeleo ya jamii ili waende kuisaidia serikali katika miradi ya kimkakati inayotekelezwa. 

Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi,amesema licha ya bodi kuwa namafaniko ya kuwafikia watu kupitia njia ya mtandao imekuwa na changamoto zinazowakabili ikiwemo kukua kwa teknolojia watu wamekuwa wakitumia mtandao wa bodi kutangaza ajira kitu ambacho kinaleta taswira mabaya kwa jamii. 

“kutoka na teknolojia kukua kuwekuwa na watu wasio waadilifu wanatumia kudanganya umma na kutangaza ajira kitu ambacho sio sahihi na imekuwa changamoto kwetu licha ya bodi kufanikiwa kuweza kuwafikia watu wengi na kurahisisha upatikanaji wa ajira,”amesema 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bibi Sophia Kaduma amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo na Mhe. Mchengerwa kwa kuwateua Wajumbe wa Bodi yake. 

Bi. Kaduma amesema kuwa watatekeleza majukumu waliyopewa kwa ufanisi na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za mchakato wa ajira ili Serikali iweze kupata watumishi watakaoweza kuleta maendeleo katika taifa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments