Waziri wa Afya Kenya: Hoteli na migahawa isiwapokee watu ambao hawajachanjwa


  • Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe
    Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe

Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Afya, imeagiza migahawa na hoteli kutotoa huduma kwa wateja ambao hawajachanjwa kama njia ya kukabiliana na maambukizi ya COVID-19 nchini humo hususan katika kipindi hiki cha sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe amewaagiza washikadau wote katika sekta ya mahoteli na maeneo ya umma kuomba uthibitisho wa chanjo kabla ya kuwaingiza watu katika vituo vyao.

Amesema: "Migahawa yote na maeneo ya umma yanakumbushwa kutopokea watu ambao hawajachanjwa."

Vilevile Kagwe amewahimzia wananchi kupata chanjo ya corona kabla ya kwenda kwenye maeneo ya umma ili kuzuia maambukizi ya virusi vinavyoendelewa kuangamiza wanadamu.

Wakati huo, Waziri wa Afya wa Kenya alionya kwamba maambukizi ya COVID-19 yanaendelea kuongezeka nchini humo, huku watu 1,596 wakipatikana na COVID-19 kutokana na sampuli 4,242, zilizochukuliwa jana Jumatatu, Disemba 27. 

Taarifa ya Wizara ya Afya ya Kenya inasema jumla ya kesi zilizothibitishwa sasa zimefikia 284,150, na vipimo 2,994,912 vilivyofanywa hadi sasa.

Waziri wa Afya wa Kenya amesema kuwa, vituo vyote vya chanjo vya umma na vya binafsi vitaendelea kuwa wazi katika kipindi hiki cha sikukuu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments