Radi yaua 7 Rukwa

              

Watu saba wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi katika maoneo tofauti katika wilaya zaNkasi na Sumbawanga mkoani Rukwa.

Akizungumza na Mwananchi leo Februari 27, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nkandasi, Given Kisantola, amesema tukio la kwanza lililotokea Februari 26 saa 9 mchana kijiji cha Nkandasi wilayani Nkasi.

Amesema katika tukio hilo, watano waliokuwa wakifanya kibarua cha kupanda maharage shambani walikufa papo hapo huku 14 kati yao walijeruhiwa baada ya kupigwa radi wakiwa wamejikinga kwenye nyumba kidogo iliyopo shambani humo.

Amesema kuwa watu hao wakiwa wanaendelea na shughuli zao, baada ya kuona mvua imeanza kunyesha waliacha kupanda maharage na kuamua kukimbilia kwenye nyumba hiyo ili kujikinga na mvua.

Amesema, wakati watu hao wakiwa wamekaa ndani ya nyumba hiyo, ghafla radi ilipiga na kusababisha vifo hivyo na kujeruhi wengine waliokuwa wamejikinga mvua katika nyumba hiyo.

Mtendaji huyo amesema kuwa waliofariki ni wanaume watatu na wanawake wawili na majeruhi walikimbizwa katika zahanati ya jeshi Milundikwa kwa ajili ya matibabu na wengi wao wanaendelea vizuri huku wengine wakiruhusiwa kurudi nyumbani.

Ambao ni yusuph mbalamwezi (24), Leonard Wayomba (21) Flansisco Kangama, Fazil wayomba (24) Shukuru Mutayagwa (28) na mtoto Abinet Kazumba (8).

Amewataja pia majeruhi kuwa ni pamoja na Veronica Saanane(27), Fobi Mbonile(28) Solostina Sokoni (39), Edina Noel (39) Getruda Mwananjela (34) mtoto Tatu Miyula (10) Teddy Wazamani (37), Mary Kauzeni (18)Daniel Kamilembe (19)  Lenatha Chakula (51) Magreth Savery (40),Retisiya Fataki (38) na Veronica Swaila (27).

Aidha katika tukio jingine tukio jingine lililotokea siku hiyo hiyo mwanaume mmoja ambaye jina lake halijajulikana mkazi wa kijiji cha Luwa Manispaa ya Sumbawanga, amekufa papo hapo yeye na mtoto wake baada ya kupigwa radi wakiwa shambani wanalima.

Kamanda Polisi mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments