SPIKA TULIA : WABUNGE 19 CHADEMA WAPO KIHALALI BUNGENI

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson amesema kuwa uwepo wa Wabunge 19 wa 'Viti Maalum wa CHADEMA' ni halali na si haramu kwani wasingekuwepo bungeni.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatatu Februari 14, 2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari wanaoripoti Bunge ambapo aliulizwa kuhusu uhalali wa kuwepo kwa wabunge hao.

Akijibu swali kuhusu Swali hilo Spika Dkt Tulia amesema kuwa hadi sasa wabunge hao wapo kwa mujibu wa sheria kwani kila mbunge ni lazima atokane na chama na hao nao wametokana na chama.

Amesema Bunge halioni shida kuwaondoa wabunge na lilishawahi kufanya hivyo katika mabunge yaliyotangulia.

"Bunge la 11 limewahi kuondoa Wabunge. Mabunge yaliyopita Wabunge wameshawahi kuondolewa kwa sababu Katiba yetu inataka Mbunge awe Mwanachama wa Chama flani. Mtu akifukuzwa Uanachama, anakuwa hana Uhalali wa kuwepo Bungeni" Dkt Tulia


Ameeleza kuwa kwa sababu ya Demokrasia, Michakato lazima iwe imemalizwa na Bunge kuletewa taarifa rasmi ya Mhusika kutokuwa Mwanachama

Hata hivyo amesema mchakato wa namna gani walifika Bungeni siyo hoja ambayo Bunge linatakiwa kujibu bali wenye majibu ni tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Ameongeza kuwa taarifa itakayopelekwa bungeni kuhusiana na wabunge hao sharti iwe imekidhi vigezo vyote vinavyotakiwa kwa kutendewa haki na yeye hatakuwa na shida kwenye maamuzi.

Novemba 24, 2020 wabunge 19 wa Chadema waliapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalumu hali iliyozusha malumbano ya namna waliteuliwa na majina yao kupelekwa Bungeni kwani chama chao kilidai kuwa hakikutoa ridhaa.

Wabunge hao ni Halima Mdee, Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments