Breaking News: Basi lapata ajali Songwe


 Basi la kampuni ya Kilimanjaro linalofanya safari kutoka Tunduma kwenda Dar es Salaam limepata ajali maeneo ya Senjele mkoani Songwe.

Basi hilo limepata ajali leo Jumatatu Machi 14, 2022 asubuhi wakati likielekea Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ausi amethibitisha kutokea ajali hiyo akisema anaelekea kwenye eneo la tukio.

Bado hakuna taarifa za vifo wala majeruhi zilizoripotiwa mpaka sasa.

Kamanda Ausi ameahidi kutoa taarifa baadaye

Endelea kufuatilia bandolamedia.co.tz kwa habari zaidi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments