Moderna kujenga kituo cha kutengeneza chanjo nchini Kenya

Ripoti zaidi zinaeleza kuwa, kituo hicho kikiwa tayyari kinatarajiwa kutoa hadi dozi milioni 500 za chanjo kila mwaka.

Mpango huo umesifiwa kuwa utasaidia kutatua upatikanaji wa chanjo katika janga la sasa la virusi vya corona na katika milipuko ya siku zijazo. Moderna inatarajia kuwekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 500 katika kituo hicho huko nchini Kenya.

Hayo yanajiri katika hali ambao mwezi uliopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa, nchi sita za Afrika zimechaguliwa kuanza utengenezaji wao wa chanjo za Covid-19 kwa kutumia teknolojia ya mfumo wa mRNA.

Serikali ya Kenya imetia saini mkataba na kampuni ya teknolojia ya kibayoteknolojia ya Marekani, Moderna Inc kwa ajili ya kujenga kituo cha kutengeneza chanjo katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

 Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, Senegal, Misri na Tunisia zimechaguliwa kuwa nchi za kwanza kupokea teknolojia ya mRNA kutoka kituo Shirika la Afya Duniani (WHO) cha kimataifa, katika bara hilo ambalo, kwa kiasi kikubwa limeendelea kukabiliwa na changamoto za upatikanaji wa chanjo za ugonjwa huo.

Viongozi mbalimbali wa Mataifa ya Afrika wameendelea kulalamikia ubaguzi wa utoaji chanjo za kupambana na virusi vya Corona, unaofanywa na mataifa tajiri duniani.

Aidha Umoja wa Afrika AU umetoa taarifa mara kadhaa ukilalamikia ugavi usio wa kiadilifu wa chanjo za ugonjwa wa Covid-19 duniani na kusisitiza kuwa unatiwa wasiwasi na uhaba wa chanjo hizo katika baadhi ya nchi maskini duniani.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments