SIMBA SC KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA, YACHAPWA 3-0 DHIDI YA ASEC MIMOSES

 

KLABU ya Simba imeshindwa kutamba kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupokea kichapo mabao 3-0 dhidi ya ASEC Mimoses .

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya aina yake ambapo licha ushindi walioupata ASEC Mimoses kipa wa Simba Sc Aishi Manula ameweza kuokoa hatari nyingi ikiwemo penati mbili katika kipindi cha kwanza na cha pili.

Mabao ya ASEC Mimoses yamewekwa kimyani na mshambuliaji Stephene Aziz Ki, Aubin Kramo pamoja na lingine likifungwa na Karim Konate.

Simba Sc itasubiri mechi yake ya mwisho wakiwakaribisha US Gendermerie mchezo ambao utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments