TUUNGE MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA MAENDELEO YANAKUJA - LUBINGA

 Wananchi na Watanzania wametakiwa kuendelea kuiamini na kuiunga Mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo inaendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi  kwa kuwaletea Watanzania Maendeleo.


Wito huo umetolewa na Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga Katibu wa NEC ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,  aliyemuwakulisha Katibu Mkuu CCM Taifa Ndg. Daniel Chongolo, Wakati wa Sherehe za kujipongeza  Wanachama wa CCM Wilaya ya Bukoba Vijijini kwa Ushindi walioupata Uchaguzi Uliopita, sherehe hizo zikifanyika Kijiji cha Msira Kata Katoro Jimbo la Bukoba Vijijini Machi 01, 2022.

Kanali Mstaafu Ngemela amewakumbusha kuwa Dhamila ya  Chama chochote cha Siasa ni Kushika Dola na kuwaletea Wananchi wake maendeleo, na hivyo kazi ya CCM chini ya Rais Samia ni kusogeza Maendeleo kwa Watanzania

"...CCM ndio inayoulizwa maendeleo yako wapi, na ndiyo inayoulizwa mlituahidi nini na ndio Maana CCM inatimiza wajibu wake, naomba madiwani msimamie miradi maendeleo kwenye Kata zenu, madiwani mna dhamana kubwa na msiwaamini watendaji wa Halmashauri.." amesisistiza Katibu Lubinga.

 Naye Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Jasson Rweikiza amewashukuru Wananchi wa Katoro kwa kurejesha Kata hiyo Mikononi mwa CCM baada ya kuwa upinzani kwa Miaka 15, ambapo kwa kurejesha Kata hiyo, tayari maendeleo mbalimbali yameanza kuonekana  ikiwemo Miradi ya Barabara, Maji, huduma za Afya ambapo pamoja na mambo mengine Dkt. Rweikiza ameahidi kuchangia Milioni kumi katika Ujenzi wa  Zahanati ya Kijiji Msira.

Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akipokea Tunda aina ya Boga Miongoni mwa zawadi alizopewa na Wananchi wa Katoro.

sehemu ya Wananchi waliohudhuria Sherehe za CCM katika Jimbo la Bukoba Vijijini wakiendelea kufuatilia Matukio


Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akizungumza na Wananchi Kata Katoro Jimbo la Bukoba Vijijini wakati wa Sherehe za CCM.
Bi. Costancia Nyamwiza Buhiye Mwenyekiti wa CCM Mkoa kagera akitoa Nasaha zake kwa Wana Katoro
Dkt. Jasson Samson Rweikiza Mbunge wa Jimbo la Bukoba akizungumza na Wanajimbo wake,  wapiga Kura na Viongozi waliohudhuria Sherehe za CCM Katoro.
 
Na Abdullatif Yunus Michuzi Kagera.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments