UN: Watu milioni 500 hawana usalama wa maji barani Afrika

Umoja wa Mataifa umesema watu zaidi ya milioni 500 katika nchi 19 za bara Afrika wanasumbuliwa na ukosefu wa maji safi na salama.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Mazingira ya Maji na Afya yenye makao yake Canada, na ripoti yake kuchapishwa jana Jumatatu na Umoja wa Mataifa kwa mnasaba wa Siku ya Maji Duniani umeonyesha kuwa, ghairi ya Misri, nchi nyingine zote za Afrika zinakumbwa na ukosefu wa usalama wa maji kwa kiwango kisichopungua asilimia 30.

Utafiti huo umeonyesha kuwa, nchi 19 za Afrika zina usalama wa maji chini ya kigezo cha asilimia 45 cha UN, huku Somalia, Chad na Niger zikiongoza katika orodha ya nchi za Kiafrika zinazosumbuliwa sana na uhaba au ukosefu wa maji safi.

Grace Oluwasanya, mtafiti mkuu wa Taasisi ya Mazingira ya Maji na Afya ya Canada amesema: Kwa ujumla, usalama wa maji katika nchi za Afrika upo chini ya viwango. Hatua za dharura zinapaswa kuchukuliwa.

Mgogoro wa maji duniani
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, ukosefu wa maji safi na salama unaweza kuua watoto walio na umri wa chini ya miaka 5, mara 20 zaidi kuliko mabomu na risasi katika maeneo ya kivita.

UNICEF inasisitiza kuwa, watoto walio dhaifu sana wapo katika hatari mara nane  zaidi kufariki dunia kama watakosa maji safi na salama ikilinganishwa na watoto waliozaliwa katika mazingira ambapo maji yanapatikana vizuri.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments