Makamba Akumbushia Misukosuko Maliyopitia Na Kinana, Ataka Awasamehe Wote

 

  Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba amemuomba Makamu Mwenyekiti wa CCM aliyechaguliwa Abdulrahman Kinana kusahau yaliyopita na kusamehe.

Makamba amesema kuwa yeye na Kinana waliwahi kunyeshewa mvua kwa kuitwa kwenye kamati ya maadili na yaliwakuta huko.

Amesema kiongozi mwenye busara na hekima huwa anasamehe hivyo angetamani kuona kiongozi huyo akiwasamehe waliokuwa wamewashughulikia ambao baadhi amesema wapo kwenye mkutano.

"Leo yameisha, wewe ndiyo bosi wao hivyo nenda ukawaongoze, jenga tabia ya kusamehe na kuwasamehe maana na wengine wapo hapa," amesema Makamba.

Kinana na Makamba waliwahi kuitwa kwenye kamati ya maadili ya CCM chini uongozi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli na Katibu Mkuu, Dk Bashiru Ali.

Kamati hiyo ilikuwa ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula ambaye jana aliandika barua ya kung'atuka ndipo nafasi yake ikachukuliwa na Kinana.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kabla ya kufungua Mkutano huo Maalum wa dharura uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 01 Aprili, 2022.

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga kura kwa ajili ya kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa upande wa Tanzania Bara Abdulrahman Kinana katika Mkutano Mkuu wa dharura uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 01 Aprili, 2022.

        

Viongozi mbalimbali wa Chama pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa ndani ya ukumbi wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kupitisha marekebisho ya Katiba ya Chama ya mwaka 1977 pamoja kumpigia kura kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana leo tarehe 01 Aprili, 2022.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments