Wagonjwa Wa Mwisho Wa Corona Waruhusiwa Kurejea Nyumbani Nchini Uganda

Akizungumza katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na gazeti la kila siku la Daily Monitor la nchi hiyo, msemaji wa Wizara ya Afya ya Uganda, Emmanuel Ainebyoona amesema, wananchi wanapaswa kuendelea kuchukua hatua zote za kujikinga na corona licha ya kutobakia mgonjwa yeyote wa UVIKO-19 katika hospitali za nchi hiyo. Amesema, uwezekano wa kuzuka wimbi jingine la maambukizi ya ugonjwa huo bado ni mkubwa.

Amesema, hivi sasa hakuna mgonjwa yeyote wa corona aliyelazwa hospitalini nchini Uganda, lakini bado kuna watu wenye ugonjwa huo nchini humo na hilo linafanya hatari ya kuzuka wimbi jingine kuwa kubwa la maambukizi ya UVIKO-19.

"Tunapaswa kuchukua tahadhari kubwa hasa kwa kuzingatia kuwa baadhi ya nchi bado zina karantini ya corona kutokana na kuzuka upya wimbi la maambukizi ya ugonjwa huo," amesema kwa kusisitiza.

Takwimu za karibuni kabisa za Wizara ya Afya ya Uganda zinaonesha kuwa, katika kipindi cha baina ya tarehe 12 hadi 14 mwezi huu wa Aprili, kuliripotiwa kesi 27 za corona nchini humo. Kiwango hicho ni cha maambukizi ya chini kabisa ya asilimia 0.3 ikiwa na maana kwamba janga la corona limedhibitiwa nchini Uganda. Viwango vya kimataifa vinasema kuwa, kesi za ugonjwa wowote zilizo chini ya asilimai 5 huwa na maana janga la ugonjwa huo limedhibitiwa.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments