MAYELE ATETEMA CCM KIRUMBA, YANGA SC IKILAZIMISHWA SARE NA BIASHARA UNITED

 

KLABU ya Yanga imelazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Biashara United ya Mkoani Mara kwenye mchezo wa ligi kuu NBC uliochezwa katika dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya aina yake maana mikikimikiki iliyokuwa ni yakutosha hasa kwa upande wa Yanga ambao walionekana kuwa mwiba dhidi ya wapinzani wao Biashara United kwenye mchezo huo.

Yanga Sc imejaribu kutengeneza nafasi nyingi za wazi lakini wachezaji wao hasa washambuliaji hawakuwa makini kumalizia mipira ambayo ilikuwa inatengenezwa na viungo wao wa pembeni.

Fiston Kalala Mayele anaendelea kuonesha uwezo wake wa upachikaji wa mabao baada ya leo hii kufunga bao kali ambalo lilimshinda kipa wa Biashara United na kutinga moja kwa moja wavuni.

dakika chache tu baada ya Mayele kupachika bao mnamo dakika ya 74 ya mchezo, Biashara nao wakasawazisha bao na kuwafanya waambulia pointi moja kwenye mchezo huo.

Kwasasa Mayele atakuwa na mabao 14 sawa na George Mpole mchezaji wa Geita Gold katika kinyang'anyiro cha ufungaji bora wa ligi hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments