SIMBA SC: HATUSHIKIKI, WALA HATUZUILIKI

 Klabu ya Simba rasmi imezindua Wiki ya Simba jijini Dar es Salaam kuelekea kilele cha ‘Simba Day 2022’ ambayo itakuwa Agosti 8, mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiwa ni miaka 13 sasa tangu kuasisiwa mwaka 2009.


Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez amesema msimu ujao wa mashindano watakuwa hawashikiki, hawazuiliki (We are Unstoppable) kama kauli mbiu ya tamasha hilo inavyosema.

Barbara amesema msimu ujao wanaingia kibabe zaidi kuhakikisha wanabeba tena ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho (ASFC), Ngao ya Hisani na kufika Nusu Fainali ya Michuano ya Kimataifa.

“Tunaingia kibabe zaidi, tutapambana ili kutetea ubingwa wetu tuliopoteza na mataji mengine yote, kuanzia wiki ijayo tunaanza kutangaza Wachezaji wengine ambao tumewasijili kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano”, amesema Barbara.

Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Murtaza Mangungu amesema watahakikisha wanafanya usajili mzuri, ili kufanya vizuri kwenye msimu huo, pia amesema Jezi zao za msimu ujao zinatoka barani Ulaya na sio barani Asia.

Naye, Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Mzee Hassan Dalali amesema mwaka huu wanatimiza miaka 13 tangu kutambulishwa kwa tamasha hilo mwaka 2009, amesema wanajivunia mengi ambayo wamefanya.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments