Recent-Post

TAWA YATOA ELIMU KWA VIJIJI VINAVYOPAKANA NA PORI TENGEFU KILOMBERO

 Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kupitia Maafisa Ujirani Mwema imetoa elimu kuhusu umuhimu wa shughuli za uhifadhi kwa vijiji vinavyoizunguka Pori Tengefu Kilombero.

Vijiji vilivyoweza kupatiwa elimu ni pamoja na vijiji vya Apera Asilia, Madibira, Sofi Majiji na Kipenyo vilivyopo wilaya ya Malinyi. Vilevile vijiji vya Minepa na Mazimba vilivyopo wilaya ya Ulanga, vijiji vyote hivi vinapatikana katika Mkoa wa Morogoro.

TAWA inaendelea na kampeni nyake ya kuelimisha wananchi waishio pembezoni mwa Pori Tengefu Kilombero kuhusu umuhimu wa eneo hilo kiikolojia, kijamii na kiuchumi.
Post a Comment

0 Comments