Imamu wa msikiti asimamishwa kwa kutosoma taarifa ya fedha

 

Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Kilimanjaro limemsimamisha Imamu wa msikiti wa Nkwekola Mudio wilayani hapa, Imrani Kimaro kwa madai ya kutokusoma mapato ya msikiti kwa miaka saba.

Mbali na kumsimamisha Imamu huyo pia, Baraza hilo limezisimamisha kamati mbili za misikiti ya zamani na ya sasa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Katibu wa Bakwata Mkoa wa Kilimanjaro, Awadhi Lema, ametoa taarifa hiyo leo Machi 5 baada ya swala ya Ijumaa, akisema wamelazimika kufikia uamuzi huo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo na kurudisha amani ndani ya msikiti huo


"Ni kweli tumeusimamisha uongozi mzima wa msikiti huu baada ya waumini kulalamikia kutokusomewa mapato na matumizi ya miaka saba.

“Pia msikiti unaongozwa na ndugu, huku kukiwa na makundi mawili yanayohasimiana, jambo liloashiria kuwepo na uvunjifu Amani," amesema Lema

Amesema February 28 mwaka huu, msikiti huo ulio chini ya taasisi ya Islamic Solidarity Center, ulimwandikia arua ya maombi Sheikh wa mkoa, Shaabani Mlewa ukimwomba kuingilia kati mgogoro huo baada ya wao kushindwa kuusuluhisha.

"Walituomba kusaidia mgogoro huo ili umalizike baada ya kuzuka makundi mawili msikitini na kuanza kutishiana na kurushiana maneno yasiyofaa na wengine kumtishia immamu.

“Leo Baraza la Masheikh limefika na uamuzi wa kuusimamisha uongozi mzima kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili Viongozi wa Msikiti huu," amesema Lema.

Desemba 25 mwaka jana, Mwenyekiti wa Baraza la Ulamaa mkoani humo, Sheikh Yusufu Ismail aliagiza misikiti 12 iliyo chini ya Islamic Solidarity Center ichague viongozi. 

Imeelezwa kuwa kabla ya uchaguzi huo kufanyika, viongozi walitakiwa wasome kwanza mapato na matumizi, lakini msikiti wa Nkwekola hawakusoma na hivyo kukwamisha uchaguzi.

"Msikitini kumekuwa na vurugu kubwa na kila mtu ana watu wake, tumesuluhisha ikashindikana, malalamiko yalipelekwa kwa Mkuu wa Wilaya Hai na pia Bakwata na ndiyo wamefika hapa na kuomba kukutana na pande zote mbili," amesema Ismail

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments