Recent-Post

Hawa Simba wana balaa

 

BAADA ya kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Luis Miquissone, Simba sasa imefikisha idadi ya wachezaji tisa waliosajiliwa kwa ajili ya msimu wa mwaka 2023/24.

Wachezaji wengine ambao mpaka sasa wamesajiliwa ni Che Malone, Shaabani Iddi, Fabrice Ngoma, Abdallah Hamis, David Kameta, Essomba Onana, Aubin Kramo na Hussein Kazi.

Simba inakabiliwa na wingi wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Africa Super League, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.

Licha ya wachezaji hao, pia Simba inaelezwa kuwa ipo katika harakati za kutafuta kipa mwingine atakayesaidiana na Aishi Manula pamoja na Ally Salim.

Post a Comment

0 Comments