Hai wampa mzabuni kukusanya mapato kudhibiti upotevu

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Edmund Rutaraka ameeleza zababu ya kumpa mzabuni kazi ya ukusanyaji wa mapato, akisema ni baada ya vijana waliokuwa wamepewa kazi hiyo kushindwa.


Akizungumza jana Agosti 4, 2023, Rutaraka wakati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani, amewataka madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo kuwa na jicho la tatu katika makusanyo ya mapato ya ndani yanayokusanywa na wazabuni huyo.

"Sisi tumeona wale vijana waliokuwa wanafanya kazi kama vibarua ya kukusanya mapato, walikuwa hawatumii mashine za kieletroniki walizopewa na Halmshauri, tumefutilia tukaona pesa tunayokusanya ni ndogo na tukaamua kuanzia sasa kuweka wazabuni,” amesema.

Amesema awali waliunda timu ya wataalamu kufanya tathimini kwa vipindi tofauti sehemu yenye miradi mikubwa.

“Kwa hiyo tuliona tunapokuwa na timu za uangalizi, mapato yanaongezeka na ndiyo tukaona sasa wazabuni watusaidie kukusanya tuweze kufikia lengo tuliloliweka," amesema.

Amebainisha kuwa wakati vijana waliowekwa awali kukusanya zaidi ya Sh230 milioni katika chanzo cha Cemichemi ya Chemka, mzabuni wa sasa ameingia makubaliano ya kukusanya Sh360 milioni.

Kwa upande wake, Mkurungenzi Mtendaji wa Halmshauri hiyo, Dionis Myinga, amesema watashirikiana kwa pamoja kusimamia ukusanyaji wa mapato hayo ili pesa hizo ziende kutekeleza miradi ya wananchi na kutoa huduma muhimu za jamii kama afya na elimu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments