Kishindo cha siku ya mwisho dirisha la usajili Ulaya

 

WAKATI Saa kadhaa zikisalia kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya kuna baadhi ya sajili zinatarajiwa kutikisa katika siku ya mwisho ya dirisha hilo, Dirisha hilo kubwa la usajili linatarajiwa kufungwa usiku wa leo Septemba 01, 2023.

Moja ya sajili zinazotizamwa zaidi ikiwa zitakamilika ni uhamisho wa Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah ambaye anahusishwa na klabu kutoka Saudi Arabia, Je Salah atanasa kwenye Mtego wa matajiri hawa kwenye soka? Majibu yatapatikana baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili usiku wa leo.

Kinda Ansu Fati anatarajiwa kujiunga na Brighton kwa mkopo akitokea Barcelona baada ya kuelezwa kuwa ameikataa klabu ya Tottenham hotspur na huenda usajili huo wa mkopo mwa mwaka mmoja ukakamilika siku ya mwisho ya usajili.

Joao Cancelo nae anatarajiwa kujiunga na Barcelona akitokea Manchester City kwenye siku ya mwisho ya usajili imeelezwa kuwa tayari Barcelona wamekwisha malizana na Cancelo na kilichosalia ni makubaliano ya klabu hizo mbili yaani Barcelona na Manchester City.

Manchester United wanatarajiwa kukamilisha sajili mbili katika saa zilizosalia kabla ya dirisha la Usajili kufungwa ambapo baada ya kuamua kuweka nguvu kwenye dili la mlinzi wa kushoto wa Tottenham Hotspurs Sergio Regulion kuna uwezekano sasa wakuipata pia saini ya kiungo wa Fiorentina Sofian Ambrabat ambaye amekuwa akiwindwa vikali na mashetani hao wekundu wa Old trafford.

Tofauti na inavyodhaniwa kuwa aliyekuwa nahodha wa Manchester United Harry Maguire ataondoka klabuni hapo ni kwamba uwezekano wa Maguire kuondoka ni mdogo mno baada ya kuumia kwa mlizi Raphael Varane hivyo united wanahofia kumuuza Maguire.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments