Bashungwa atoa maagizo kwa Mameneja TANROADS

TANGA; Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewaagiza mameneja wa wakala wa barabara TANROADS katika mikoa inayopakana na barabara kuu ya Chalinze hadi Arusha kushirikiana kufanya ukarabati wa barabara hiyo ili kukabiliana na changamoto ya uharibifu.
Rai hiyo ameitoa wakati akikagua hatua za dharura za ukarabati wa barabara zilizochukuliwa na TANROADS katika eneo la Bwiko wilayani Korogwe mkoani Tanga katika barabara kuu ya Pwani kuelekea Kilimanjaro ambapo jana palipatwa na athari kutokana na mvua kubwa za El-nino zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali.
Amesema kuwa kutokana na barabara hiyo kuwa ndio kiungo muhimu kwenye sekta ya usafirishaji ikiwemo nchi za jirani hivyo ni vema Mameneja wa mikoa hiyo wakatenga bajeti ya kufanya marekebisho ya mara kwa mara.
“Niwaagize Mameneja wa Mikoa ya Pwani,Tanga, Kilimanjaro na Arusha tengeni fedha kwa ajili ya kuhakikisha barabara hii inafanyiwa marekebisho ya mara kwa mara ili iweze kuwa imara kipindi chote cha misimu”amesema Bashungwa.
Aidha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini Mhandisi, Mohamed Besta amesema wataimarisha usimamizi wa miradi ya barabara ikiwemo na usanifu Ili kupata barabara zenye viwango bora.
“Kumekuwa na changamoto ya barabara mpya kuharibika katika kipindi cha uangalizi hivyo tumejipanga kuhakikisha tunapata wakandarasi mahiri lakini na kuimarika wakati wa usanifu wa miradi kabla haijaanza utekelezaji wake”amesema Mhandisi Besta

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments