Tusubiri mechi mbili za mwisho
IMEBAKI michezo miwili kufahamu mustakabali
wa Tanzania katika kundi F, baada ya leo kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya
Morocco.
Katika mchezo huo uliopigwa muda mchache
uliopita uwanja wa Laurent Pokou San Pedro, Stars imepoteza mabao 3-0.
ISOME NA HII >TFF: Kauli Za Amrouche Hatuzitambui
Mabao ya Morocco yamefungwa na Roman Saiss,
Azzedine Ounahi na Youssef En-Nesyri.
Stars sasa itasubiri mchezo unaofuata dhidi
ya Zambia utakaochezwa Januari 21, 2024 katika uwanja huo.
Mchezo wa mwisho wa kumaliza hatua ya
makundi, Tanzania itakutana na DR Congo Januari 24.
Ili kufufua matumaini ya kusonga 16 bora, Stars inapaswa kushinda mchezo unaofuata dhidi ya zambia.
0 Comments