GOMES AWATAKA WACHEZAJI WAWE MAKINI KWENYE MIPIRA ILIYOKUFA


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ni lazima wachezaji wake wawe makini kwenye matumizi ya mipira iliyokufa ili kupata matokeo chanya.

Simba ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Al Merrikh kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Mchezo wao uliopita uliochezwa Uwanja wa Al Hilal walilazimisha sare ya bila kufungana hivyo wana kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo huo ili kukata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Ikiwa ipo kundi A iliweza kushinda mchezo wa kwanza mbele ya AS Vita ugenini kwa bao la penalti lilifungwa na Chris Mugalu na ilishinda mbele ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa kwa bao la Luis Miquissone.

Kwenye mchezo wao uliopita ambao ni wa ligi, Mugalu alikwama kuzamisha nyavuni penalti baada ya kipa wa Tanzania Prisons, Jeremia Kisubi kuipangua na kuifanya kuwa kona.

Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na kuzifanya timu hizo kugawana pointi mojamoja.

Gomes amesema:"Nimekuwa nikiwaambia muda mwingi kwamba wana kazi ya kutumia vizuri hii mipira ya kutengwa ili wawe wanapata matokeo mapema hivyo ni muhimu kufanya vizuri.

"Kwenye mazoezi hilo tumekuwa tukifanyia kazi mara kwa mara hivyo nina amini kwamba kwa mechi zetu zijazo kutakuwa na mabadiliko zaidi," .

Mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa Jumanne mashabiki wamezuiwa kuingia kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Soka Afrika, (Caf).

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments