Recent-Post

VYAMA VYA WAFANYAKAZI VYATAKIWA KUJITATHMINI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye ulemavu) Mh Jenista Mhagama amevitaka Vyama vya wafanyakazi kujitathini katika utekelezaji wa majukumu yao kuhakikisha kunakuwa na utulinvu endelevu maeneo ya kazi.

Waziri Mhagama aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akifungua  mkutano wa siku mbili wa mashauriano kati ya Serikali, na wadau wa sekta ya usafirishaji alisema Chama cha wafanyakazi kina kinapaswa kusimama imara kuondoa migogoro na siyo kuwa sehemu ya migogoro hiyo.

Mh Mhagama Aliwataka wafanyakazi,waajiri na vyama kuketi pamoja kuzungumza tofauti zao kupata muafaka utakaosaidia wafanyakazi kufanya kazi zao katika mazingira salama huku akivisisitiza vyama kuheshimu katiba,kanuni na maudhui ya lengo la vyama hivyo kuanzishwa.

“Hofu ya uwepo wa vyama vya wafanyakazi katika maeneo ya kazi imepitwa na wakati huko nyuma wakati mwingine vilitumika kama chachu ya kuanzisha migogoro kati ya mwajiri na mfanyakazi lakini katika kipindi hiki cha miaka mitano kumekuwa na utulivu wa kutosha ambao umevipelekea vyama hivyo kujipanga na kutumika kama daraja,”alisema Waziri Mhagama.

Pia aliamuagiza Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri Pendo Berege kuitisha upya mkutano wa pamoja utakaohusisha wafanyakazi wakiwemo madereva,waajiri na wadau ili kusikiliza kero za kila upande na hatimaye kupata suhulu ya malalamiko yao hatua itakayo saidia kuongeza kasi ya uzalishaji na kuinua uchumi wa Taifa.

“Hakuna haja ya kugombana wala kulumbana sheria zetu za kazi zinatuweka katika dhana ya utatu Serikali,Mfanyakazi na Mwajiri mkutano huu ni muhimu tuwe wawazi tukitulia tukayatazama malalamiko ya wafanayakzi ni yapi, malalamiko ya waajiri sekta ya usafirishaji ni yapi kwa hiyo unayakuta pande zote mbili hakuna marefu yasyikuwa na nch kila mmoja anaytakiwa apate haki yake mkutano huu urudiwe upya,”alieleza Waziri huyo.

Alionesha kukerwa na tabia ya baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri kutotoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao akisema ni kosa kisheria kwani hunyima haki zao muhimu.

“Nafikiri kikao hiki kitumike kujitathimini na kujitafakari madereva wanalalamika kila siku hawana mikataba n ani kweli katika wafanyakazi amabao hawana mikataba nchi hii ni madereva kuna siri gani kati ya hawa watu ni tatizo gani ambalo haliwezi kutatuliwa, haiwezekani tumesimamia, tumechukua hatua lakini bado sasa sijui ni madereva hawataki au wamiliki tujue kwa sababu zipi?,”alifafanua Waziri Mhagama.

Sambamba na hayo Mh Mhagama alihimiza majadiliano hayo kuwa yenye muafaka chanya na kupata suluhu ya kudumu katika sekta ya usafirishaji akisema kwamba moja ya sekta inayoongoza kuchangia mapato ya serikali ni usafirisha hivyo ni lazima ithaminiwe na kuheshimika.

Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri Pendo Berege alisema amepokea maagizo hayo na wako tayari kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa kusimamia sheria na utaratibu lengo kuu ni kuongeza thamani ya sekta ya usafirishaji. 

Na Kadala komba, Dodoma. 

Post a Comment

0 Comments