Profesa Lipumba asema Samia ameonyesha mwelekeo

 

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hotuba aliyoitoa bungeni mjini Dodoma Aprili 23, 2021  akisema imejaa faraja na kuonyesha mwelekeo.

Akizungumza jana Aprili 27, 2021 mkoani Dar es Salaam, Profesa Lipumba amesema hotuba hiyo imeonyesha jinsi rais huyo anavyojiamini.

Kuna methali ya Kiswahili inayosema ‘maneno mazuri humtoa nyoka pangoni.’ Hotuba yake imeanza kwa shukrani kwa Bunge, marais wastaafu waliomuibua kwanza na umma wa Zanzibar na baadaye Jamhuri ya Muungano,” amesema Profesa Lipumba.Akifafanua zaidi, Profesa Lipumba amekosoa maoni ya watu waliohoji kwa nini Rais Samia hakuzungumzia masuala ya haki za binadamu na kubakwa kwa demokrasia katika miaka mitano iliyopita.Binafsi sikutegemea atafanya hivyo. Anawajibu wa kuwaunganisha asionekane anaegemea kundi lolote kati ya makundi yanayokinzana. Mimi nimetiwa moyo na serikali ya awamu ya sita itakuwa inadumisha mazuri ya awamu zilizopo na  kuyaendeleza mema yaliyoachwa na kuletea mengine mapya.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments